1:DIAMOND PLATNUM ni msanii namba moja alie tajwa kwenye listi hii
ambaye ndiye anaeoongoza kwa kulipwa pesa nyingi zaidi kwenye show zake
ambapo analipwa hadi dola $4000 kwa show sawa na shilingi 350,000....
pia diamond anamiliki magari ya samani maduka nyumba na mashamba hapa
tanzania
2:PROFESOUR JAY ni msani namba mbili katika listi hii ambae ameanza
mziki miaka ya tisini nana hadi sasa ameweza ku meintane na kuedelea
kubaki kwenye game anamiliki nyumba ya kifahari yenye studio ndani pia
ana miliki mashamba na amewekeza kwenye sekta mbli mbali
3:LADY JAY DEE anashika anashika namba tatu kwenye list hii ni msanni wa
kike anaye heshimika zaidi tanzania na ameanza mziki mwishoni mwa miaka
ya tisini na amejipatia mafanikio makubwa kutokana na bidii yake kwenye
kazi ana miliki magari kibao yakiwemo toyota murano,toyota costa
minbus,toyota prado nk..ana ishi kwenye nyumba yake ya kifahari na pia
anamiliki bend yake mwenyewe machozi band
4;AMBWENE YESAYA (AY) japo kua ni mtu wakutopenda kujionesha sana lakini
ni msanii mwenye mafanikio makubwa sana Tanzania alianza mziki mwaka
2000 akiwa na kundi la eastcoast kabla ya kujitoa na kuanza kufanya kazi
zake binafsi kama solo artist anamiliki maduka kazaa ya nguo yenye
brand yake pamoja na magari yakutosha na anapiga show nyingi za nje ya
nchi ambazo zinamuingizia kipato kikubwa pia ay anamiliki kampuni ya
Unity Entertainment ambayo ina manage wasanii kama ommy dimpozi,vannesa
mdee,feza kessy na wengineo pia kampuni yake ndio inyotengeneza kipindi
cha mkasi kinachorushwa na channel 5 (east africa television)
5:JUMA NATURE (KIROBOTO) ni msanii mkongwe katika game ya bongo flaver
ambae amepata mafanikio makubwa kwenye game hii ambapo anamiliki tax
nyingi hapa daresalam pia anamiliki nyumba pamoja na mashamba
1. Kufuata mkumbo, kutokuwa na maamuzi yako mwenyewe. 2. Kuongea lugha
chafu, huwezi kumaliza sentensi bila matusi. 3. Kuvaa mlegezo. 4. Kunyoa
panki, kiduku au kuacha afro. 5. Kuvaa viatu vya four angles au vyenye
soli kubwa. 6. Kukimbia mimba au k
Ndoa nyingi zina changamoto lakini nimegundua ukioa single mother au
dada ambae ni 35+ hawa watu mara nyingi huwa ni wife materials
ukilinganisha na hawa wenye age ya 20-35. *Hawa watu wana commitment
sana katika ndoa zao. *Wanakuwa washapitia chang
Mwanaume mmoja ajulikanaye kwa jina la Saidi amenaswa na Kamera
akielezea jinsi anavyompagawisha mpenzi wake wa kiume, alikuwa akipiga
stori na Mashosti zake wa Kike..
Angalia Video Hapa chini
MWANAMUZIKI mwenye vituko kila kukicha Bongo, Baby Joseph Madaha,
ametoa dukuduku lake la moyoni na kusema kuwa kila kukicha anayatamani
mapenzi ya Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ kama angekuwa yeye.
Akizungumza na paparazi wetu, Baby alisema kuwa kila akiwaona Wema na
Diamond anatamani sana na yeye awe kwenye uhusiano wenye kupendwa na
kuhamasisha kama ulivyokuwa wa mastaa hao kiasi ambacho amefikia hatua
ya kuwaonea wivu.
“Kiukweli nikiwaona hawa watu nasikia mpaka wivu na kuna wakati
natamani niwe mimi jamani maana sifikiri kama kuna ‘kapo’ kali hapa
Bongo kama hii jamani, naitamani hadi basi,” alisema Babyalisema
Ndoa nyingi zina changamoto lakini nimegundua ukioa single mother au
dada ambae ni 35+ hawa watu mara nyingi huwa ni wife materials
ukilinganisha na hawa wenye age ya 20-35. *Hawa watu wana commitment
sana katika ndoa zao. *Wanakuwa washapitia chang
Ndoa nyingi zina changamoto lakini nimegundua ukioa single mother au
dada ambae ni 35+ hawa watu mara nyingi huwa ni wife materials
ukilinganisha na hawa wenye age ya 20-35. *Hawa watu wana commitment
sana katika ndoa zao. *Wanakuwa washapitia chang
Shirika la
afya duniani limesema kuwa zaidi ya watu elfu tatu sasa wamedaiwa
kufariki kutokana na kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola katika eneo la Afrika Magharibi kati ya visa elfu sita vya ugonjwa huo vilivyoripotiwa.
Liberia imeathiriwa vibaya na ugonjwa huo huku WHO ikisema kuwa kumekuwa na vifo 150 vilivyotokea katika kipindi cha siku mbili pekee.
Idadi hiyo inaweza kupuuzwa kwa kuwa watu wengi wanaogopa kwenda hospitalini.
Hazina ya Fedha duniani IMF imeahidi dola millioni 130 kama msaada wa dharura kwa mataifa ya Liberia,Guinea na Sierra Leone.
Mwanamke mwenye umri wa miaka 65 mjini Bangkok, Thailand, amefariki baada ya kujirusha katika bwawa lenye Mamba katika shamba la kutunza na kuhifadhi wanyama hao karibu na mji huo.
Walioshuhudia
kitendo hicho wanasema kuwa walimuona mwanamke huyo, Wanpen Inyai,
akijirusha katika bwawa lenye Mamba katika kituo cha kuwatunza wanyama
hao cha Samut Prakarn, siku ya Ijumaa.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa jarida la The Bangkok Post. Wafanyakazi wa kituo hicho walikosa kumuokoa mama huyo.
Polisi wanasema kuwa walifahamishwa na familia yamama huyo kwamba alionekana mwenye afya duni na mwenye kusongwa na mawazo kabla ya kifo chake
Vituo vya watalii nchini humo vinasemekana kukosa mikakati ya usalama.
Polisi walithibitisha kifo cha Bi Wanpen Jumanne mchana.
Kwa
mujibu wa ripoti, Bi Wanpen alivua viatu vyake kabla ya kujirusha ndani
ya bwawa hilo, ambalo linasemekana kuwa na kina cha mita tatu.
Wafanyakazi walijaribu kutumia vijiti virefu kuwafukuza Mamba hao kwa lengo la kuwazuia wanyama hao kumshambulia mwanamke huyo.
Mapema
siku hiyo, familia ya Wanpen, ilijaribu kutoa taarifa ya kupotea kwake
la lengo la kumtafuta ingawa walifahamishwa kusubiri kwa saa 24.
Kifo
chake kinafanana na kisa kimoja kilichomkumba mwanamke aliyejiua mwaka
2002 kwa njia hiyo hiyo katika kituo cha kuwatunza Mamba.
Rais wa Marekani Barrack Obama
hii leo anatazamiwa kutangaza mpango wake wa kuwatuma wanajeshi 3,000
nchini Liberia kama njia moja ya kusaidia katika vita dhidi ya ugonjwa
hatari wa Ebola.
Wanajeshi hao watasimamia ujenzi wa vituo vipya
vya kimatibabu na pia watahusika katika utoaji wa mafunzo ya kimatibabu
kwa wahudumu.
Kumekuwa na malalamishi kwamba jamii ya kimataifa
imelegea katika harakati za kukabiliana na mkurupuko wa Ebole katika
mataifa ya Afrika magharibi.
Mataifa ya Sierra Leone, Liberia na Guinea ndiyo yaliyoathirika zaidi huku zaidi ya watu 2,400 wakiwa tayari wamepoteza maisha yao kufikia sasa.
Zaidi ya nusu ya idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huu ni raia wa Liberia.
Shirika la afya duniani (WHO) limetahadharisha kuwa huenda watu zaidi wakazidi kufariki.
Umoja
wa Mataifa (UN) unapangiwa kuzungumzia jinsi ya kukabiliana na mlipuko
wa ugonjwa wa Ebola katika mkutano unaopangiwa kufanyika huko Geneva.
Kulingana na viongozi nchini Marekani, mpango wao wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola unalenga-:
Utoaji wa mafunzo ya kimatibabu kwa wahudumu wa kiafya 500 kila juma.
Ujenzi wa vituo vya matibabu 17, kila chumba kikiwa na vitanda kumi.
Usambazaji
wa vifaa vya huduma ya afya kwa kila nyumbaKampeni ya kuwahamasisha
wananchi kuhusu jinsi ya kuwashughulikia wagonjwa wa Ebola.
Ujenzi wa kituo cha kijeshi cha pamoja mjini Monrovia kitakachotumiwa katika shughuli ya kupokea msaada kutoka kwa jamii ya kimataifa.
Wadadisi
wa masuala ya kimatibabu wamepongeza mpango huu wa Marekani huku
wengine wakitilia shaka nia ya Marekani nchini Liberia.
http://mhabariforum.blogspot.com/Kwenye show ya Fashion Rock
Aliyofanya Rapper Nicki Minaj inasemekana alikosea pozi na makalio yake
kuonekana tofauti na yanavyoonekana kwenye picha zingine na kuzua gumzo
kuwa yanaweza kuwa feki kama iliyoripotiwa miaka kadha iliyopita.
Nay wa Mitego amesema baada ya
kukamilisha ujenzi wa studio yake mpya iitwayo ‘Free Nation Production’
ameamua kumkabidhi producer wake Mr T Touch kama zawadi kutokana na kazi
ambayo amekuwa akimfanyia katika muziki wake. Akizungumza na Bongo5 jana, Nay amesema
kuwa ameamua kufanya hivyo baada ya kuona kuwa muziki unazaolishwa na
producer huyo unamwingizia pesa nyingi kuliko malipo anayompa. “Wasanii tuna maproducer ,maproducer
wetu tunajuaga kama wamekuwa hawaingizi kipato kikubwa sana tofauti na
sisi wasanii,’ amesema Nay. “Producer akikugongea ngoma moja
ukimlipa laki tatu wewe unaweza ukaingiza zaidi hata ya milioni hamsini.
Kwa producer aliyekufanyia hiyo ngoma inakuwa haimtoshi, for reel
kabisa naongea kwa mara ya kwanza kwamba studio yangu imekamilika ambayo
nampa zawadi producer wangu ambaye nilianza naye tangu… nasema nao
mpaka leo hii ngoma yangu ya mwisho ya Mr Nay, zote hapa katikati
amefanya yeye. Tumepata tuzo mara mbili, ni vitu ambavyo amefanya yeye,
nimeingiza pesa nyingi lakini hela ambayo nilikuwa namlipa ni ileile
laki mbili, laki tatu haimtoshi! Mimi nimeshaingiza zaidi ya milioni mia
moja, mia mbili.” “Kwahiyo nilichofanya nimekamilisha
studio na nimemkabidhi kama zawadi yake. Studio inaitwa Free Nation
Production. Mimi mwenyewe nitakuwa nafanyia kazi zaidi kwa sababu nahisi
nitakuwa huru zaidi, japo kuwa sio lazima nifanyie hapo lakini hii ni
kama zawadi kwa producer wangu, pia watu wengine wakihitaji kurekodi
watarekodi.” Bongo5
Polisi
nchini Uganda wanasema kuwa wamekamata kiasi kikubwa cha vilipuzi
walipokuwa wakifanya operesheni ya kutibua jaribio la shambulizi la
kigaidi la wanamgambo wa al-Shabab.
Hadi sasa, watu kumi na tisa
wamekamatwa na polisi na wanahojiwa kuhusiana na nia yao kutekeleza
vitendo vya kigaidi, kulingana na msemaji wa polisi.
Wiki
iliyopita, ubalozi ya Marekani mjini Kampala ulionya kuwa kulikuwa na
uwezekano wa shambulizi la kulipiza kisasi mauaji wa kiongozi wa kundi
hilo la Al-Shabab.
Uganda inalaumiwa kwa kutuma majeshi yake kupigana chini ya Umoja wa Afrika Amisom.
Marekani ilitangaza kuuawa kwa kiongozi wa kundi la Alshabab Ahmed Abdi Godane baada ya shambulizi la angani Septemba 2 .
Serikali inasema kuwa kundi hilo la kigaidi lilikuwa limepanga kushambuliz mji mkuu wa Kampala.
Askari walisema kuwa kundi hilo lilikuwa limepanga kufanya mashambulizi katika miji mingine mwishoni mwa wiki.
Siku ya Jumapili, Marekani ilifuta onyo lao ikidai kuwa iliamini kuwa tishio la shambulizi lilikuwa halipo tena.
Waziri
wa habari nchini Uganda, Rose Namayanja aliwasihi wananchi kuendelea
kuwa waangalifu huku serikali ikiendelea kufanya uchunguzi wa
mashambulizi yoyote yaliyokuwa yamepangwa.
Alisema kuwa watuhumiwa walikuwa wamepatikana na vifaa vinavyotumiwa katika vitendo vya kigaidi na nia yao ilikuwa wazi sana.
Malaysia imetangaza kutoa mchango wa glavu milioni 20 kwa mataifa 5 yanayopambana na homa hatari ya Ebola
Serikali ya Malaysia imesema kuwa glavu hizo zitatolewa kwa wafanyakazi wa afya nchini Liberia , Sierra Leone, Guinea, Nigeria na DRC.
Upungufu wa glavu hizo umezua wasiwasi wa kuenea kwa virusi hivyo,kwa mujibu wa maafisa wa Afya.
Nchi hiyo inaongoza kwa kutengeza glavu kwa asilimia 60 ya glavu zote duniani.
"Malaysia
inaweza kutoa mchango wake wa kipekee kukabiliana na Ebola kwa sababu
nchi yetu ni moja ya nchi zinazotengeza glovu duniani, '' alisema waziri
mkuu Najib Razak.
"tunatumai kuwa mchango wetu utasaidia kuzuia kuenea kwa Ebola na kuokoa maisha.''
Zaidi ya nusu ya vifo vinavyotokana na Ebola vimetokea Liberia tangu mlipuko wa ugonjwa huu.
Sierra
Leone, Guinea na Liberia ni baadhi ya mataifa yaliyoathiriwa vibaya
sana na ugonjwa huo ambao hadi kufikia sasa umewaua zaidi ya watu 2,400
mwaka huu. Miongoni mwa makampuni ambayo yametoa mchango huo ni pamoja na Sime Darby, Kuala Lumpur Kepong, IOI Corporation Berhad na Top Glove.
Yemi-Alade-2Mpaka sasa Yemi Alade anarekodi mbili zilizofanya vizuri Africa ambazo ni Johnny na Tangerine. Hii ni kazi ya tatu ya msanii huyu ambaye hivi karibuni alikuwa coke studio Afrika na Diamond.. Album mpya ya Yemi ni King Of Queens
Kati
ya mambo ambayo watu wengi hawatilii maanani sana ni unywaji wa pombe
wakati wa ujauzito. Nimekuwa nikiwaona akina mama wajawazito wengi
wakinywa pombe kwenye sehemu za starehe na sherehe mbalimbali. Hata
hivyo si nia ya makala hii kuwazuia kunywa pombe bali kuwapa elimu
sahihi juu ya unywaji wa pombe wakati wa ujauzito.
Baadhi
ya wataalam wanasema unywaji wa wastani wakati wa ujauzito ni kitu
ambacho kinaweza kukubalika ingawa wapo baadhi ya wataalamu wengine
wanaoamini kuwa unywaji wa hata glasi moja ya mvinyo (wine) kwa wiki
huhatarisha afya ya mtoto wako. Hata hivyo haijulikani kwa hakika, ni
kiasi gani cha pombe ni salama kwa makuzi sahihi ya mtoto wako tumboni.
Wataalamu wengi wanashauri kuacha pombe kabisa wakati wa ujauzito. Pombe
inaweza kuleta madhara makubwa kwa mtoto wako bila wewe kuhisi madhara
yake. Na yanaweza kuwa madhara ya kudumu ambayo ataishi nayo maisha yake
yote. Aidha kuna dhana imejengeka kwa baadhi ya
wajawazito kuwa, hawatakiwi kunywa pombe kali kama vodka au whisky tu
lakini ni ruksa kutumia aina nyingine za pombe. Hata hivyo dhana hii si
sahihi kwa kuwa pombe za aina zote zaweza kuleta madhara makubwa kwa
kiumbe aliye tumboni.
Kisayansi takwimu zinaonyesha kwamba unywaji sana wa pombe wakati wa
ujauzito huathiri mimba. Ni hili hutokea zaidi katika kipindi cha miezi 3
ya mwanzo (first trimester), kipindi ambacho viungo vingi vya mwili wa mtoto hufanyika (organogenesis). Nini hutokea unapokunywa pombe wakati wa Ujauzito?
Pombe
ni sumu kwa mtoto. Unapokunywa pombe inaingia moja kwa moja kwenye
mzunguko wa damu wa mama kasha hufika kwa mtoto kwa kupitia kondo la
nyuma (placenta).
Mara pombe inapoingia kwenye mzunguko wa damu wa mtoto, huathiri uwezo
wa mtoto kupata chakula, virutubisho na oksijeni ya kutosha kwa ajili ya
maendeleo ya kawaida katika ubongo na viungo vingine. Hii inaweza
kuathiri ubongo wa mtoto na ukuwaji wa viungo vya mwili kwa ujumla.
Uharibifu huu unaweza kuathiri uwezo wa mtoto kujifunza na kufikiri
pindi anapozaliwa hali ambayo itajionesha kwa matendo yake kama mtoto na
kama mtu mzima.
Aidha, utafiti umeonesha kwamba uwezo wa mimba kustahimili kiwango cha
pombe ni mdogo mno hali ambayop huathiri ufanyikaji wa viungo na ukuwaji
wake kwa kiasi kikubwa. Kwa kiasi gani mtoto wako ambaye hajazaliwa anaweza kuathiriwa na pombe? Kiwango
cha kuathirika kwa mimba kutokana na unywaji pombe unaofanywa na mama
mjamzito hutegemea sana mambo makuu matatu ambayo ni:
Kiasi cha unywaji wa pombe
hatua ya mimba yaani umri wa mimba
mara ngapi unakunywa pombe
Matatizo yatokanayo na unywaji wa pombe Baadhi
ya madhara yanayoweza kumpata kiumbe aliye tumboni kwa mama kutokana na
unywaji wa pombe kipindi cha ujauzito ni pamoja na
Kutoka/kuharibika kwa mimba
Mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mdogo
Mtoto kuzaliwa akiwa na ulemavu wa mbavu na kidari (sternum)
Mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo ya mgongo uliopinda (kibiongo) na vidole vilivyoundana
Mtoto kuzaliwa akiwa na kichwa kidogo kuliko kawaida (microcephaly)
Mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo ya pua
Kuzaliwa na matatizo ya taya
Mtoto kuwa na matatizo ya kutokuona mbali
Matatizo ya moyo kama vile moyo kuwa na tundu
Matatizo ya figo
Mtoto kuwa na ubongo mdogo na pia matatizo ya akili
Mtoto kuzaliwa akiwa na mdomo sungura (lip palate na cleft palate)
Matatizo ya kimaumbile ya masikio na ulemavu kwenye sehemu za uzazi (genital malformations).
Aina mojawapo ya kansa ya chembe nyeupe za damu (Acute Myeloid Leukemia). Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika
jarida moja la utafiti wa kansa la Marekani lijulikanalo kama Journal of the American Association for Cancer Research.
Ieleweke kuwa, madhara haya si ya muda bali ya kudumu ambayo yanaweza
kusababisha kifo kwa mtoto, malezi na makuzi ya tabu na hata hisia
mbalimbali katika maisha.
Kama wewe ni mjamzito, ni vizuri kuacha kunywa pombe. Hata hivyo
wanawake ambao walikuwa wanatumia pombe wakati wa ujauzito wasiwe na
hofu sana na habari hii. Kuna msemo uliozoeleka kitabibu kuwa ‘si kila
mvutaji wa sigara anapata kansa ingawa ukweli ni kuwa wavutaji wapo
katika
hatari kubwa zaidi’. Hali hii pia ina ukweli linapokuja suala la unywaji
wa pombe wakati wa ujauzito kwamba si kila mtoto anaathiriwa na unywaji
wa pombe ingawa hatari ya kuathirika ni kubwa zaidi. Hivyo basi ni
muhimu kwa mama mjamzito kufanya maamuzi sahihi ya maisha ya mtoto wake.Madhara ya Unywaji wa Pombe wakati wa Ujauzito