More Giniazy track

[soundcloud url="https://api.soundcloud.com/tracks/167825674" params="auto_play=true&color=ff5500" width="100%" height="166" iframe="true" /]

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Jumanne, 14 Oktoba 2014

ingia ujisomeeeeeeeeeeee>>>> Mapenzi Wanawake Wenye Hips na Shida Wanazokabiliana Nazo Kila Siku eingia

Wanawake Wenye Hips na Shida Wanazokabiliana Nazo Kila SikuWanawake wengi wenye hips , ni wanawake ambao si kwa mwanaume tu hata kwa wanawake wenzie husifia kuwa fulani kajaliwa, ki maumbile, ni kweli wana mvuto wa pekee, humwagiwa sifa nyingi za urembo, lakini pia kwa upande mwingine wa shillingi ni matati…

Jumapili, 12 Oktoba 2014

Kabula kahaba.. Kabulaa mlevi...kabula ana UKIMWI ivi ni kwelii .....................???????

mhabariforum.blogspot.commuigizaji wa kike bongo movie jini KABULA anaye tumia jina la kabulaflavor intagram amefunguka hivi kuhusu wale wanaofuatilia maisha yake.... ati kipi sija sikia kabula kahaba.... kabula mlevi... kabulaa changu doaa.....kabula ana ukimwi naombeni mseme mapya  niacheni ni pumzike

ULEVI NI SHIDAAAA.....>>>>>>>>>>>

http://mhabariforum.blogspot.com/picha hapo juu inajieleza yenyewe jinsi dada huyo alivyo pombeka na kufikia hatuaah yakutojielewaaa na wajanjaa hawakusitaa kufanya yao na kumwacha dadahuyoo mtaronii ulevi ni shidaah.

Jumatano, 8 Oktoba 2014

MCHAKATO:wa katiba mpya Tanzania

http://mhabariforum.blogspot.com/Jakaya Kikwete wa Tanzania na Rais wa Zanzibar, Dr Ali Mohammed Shein, leo jioni wakitarajiwa kukabidhiwa rasimu ya katiba iliyopitishwa na Bunge Maalum la Katiba, nchi hiyo inajikuta ikiwa katika mgawanyiko wa kisiasa ambao haujashuhudiwa kwa muda mrefu. Hassan Mhelela anatathmini mchakato mzima wa kusaka katiba mpya na changamoto zake.
Rasimu hiyo ya katiba ilipitishwa kwa kura ya ndiyo ya wajumbe wengi wa chama tawala CCM na wale wa kundi maalum, huku wajumbe wa vyama vya upinzani wakisusia na wala hawakushiriki katika kupiga kura ya mwisho
Kwa sasa imeweza kuvuka hatua kuu mbili, kinachofuata baada ya Rais Kikwete kukabidhiwa itakuwa ni kupigiwa kura ya maoni na wananchi, lakini bado barabara ya kuifikia katiba kamili imejaa visiki na utelezi.
Katika hatua hiyo bado hakuna uhakika endapo itafanyika ndani ya miezi sita iliyopangwa kwa mujibu wa sheria, au kazi hiyo itasogezwa mpaka mwaka 2016 baada ya uchaguzi mkuu wa 2015.
Lakini kizingiti kingine ambacho katiba itakabiliwa nacho ni kuoanisha katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kuendana na katiba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar – zinazounda Muungano wa Tanzania.
Ikumbukwe kuwa kabla ya mabadiliko haya kuanza mwaka jana, Zanzibar ilikuwa imefanya mabadiliko ya katiba yake mwaka 2010 kama hatua mojawapo ya maridhiano ya amani yaliyomaliza uhasama kati ya chama tawala CCM na upinzani CUF.


http://mhabariforum.blogspot.com/Swali la kujiuliza ni kwamba kutokana na msimamo wa wajumbe kutoka Zanzibar kupinga rasimu hiyo, je watakubali kufanya mabadiliko katika katiba ya Zanzibar ili iendane na rasimu inayopendekezwa, na lini litafanyika hilo?
Kimsingi ili mabadiliko ya katiba ya Zanzibar yafanyike inatakiwa ipitie katika Baraza la Wawakilishi (sawa na Bunge la Zanzibar) na baada ya hapo iidhinishwe kwa theluthi tatu ya kura ya maoni ya wananchi wa Zanzibar.
Kwa upande mwingine, maswala makubwa yaliyosababisha mgawanyiko ni muundo wa serikali – ziendelee kuwa mbili kama ilivyo sasa au ziwe tatu kama rasimu ya kwanza na ya pili zilivyopendekezwa na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Jaji Joseph Warioba?
Hapo katikati kumetokea mvurugano ambao umeacha maswali mengi zaidi kuliko majibu yanayotoa ufumbuzi – hata tume iliyokusanya maoni imekuwa imepuuzwa na wajumbe wake kurushiwa vijembe kutoka nje na ndani ya Bunge Maalum la Katiba kuwa iliegemea upande mmoja.
Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohammed Shein amemfukuza kazi aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman kutokana na msimamo wake wa kupinga rasimu hiyo ya katiba.
Nafasi yake imechukuliwa na Said Hassan Said, aliyetangazwa siku moja kabla ya rasimu kukabidhiwa kwa Rais Kikwete na Rais Shein wa Zanzibar.

http://mhabariforum.blogspot.com/Bunge la Tanzania
Huo ni msimamo ambao ni nadra sana kujitokeza hadharani katika siasa za Tanzania, na wachambuzi wa mambo wanasema haishangazi kuona hatua zilizochukuliwa.
Vile vile waliokuwa wajumbe wa tume hiyo wamekanusha kupendelea upande wowote, badala yake wameeleza kuwa walichowasilisha ni maoni ya watanzania.
Ingawa chama kikuu cha upinzani CHADEMA kimejaribu kuhamasisha maandamano ya nchi nzima kupinga mchakato huo wa katiba, hakijapata mafanikio makubwa kutokana na serikali kutumia vyombo vya dola kudhibiti maandamano hayo.
Jambo la kusubiri kwa hamu ni kuona kama Rais Kikwete atatoa hotuba itakayojaribu kuwaunganisha watanzania wakijiandaa na hatua inayofuata ya katiba, au atawapuuza wapinzani na wananchi wanaopinga rasimu hiyo.
Ikumbukwe kwamba mwezi uliopita Rais Kikwete na viongozi wa vyama vya siasa Tanzania ikiwemo chama chake cha CCM, walikubaliana kuwa mchakato wa kupata katiba mpya usimame baada ya hatua hii ya Bunge hadi baada ya uchaguzi mkuu.
Hata hivyo suala hilo pia linategemea kuzua mvutano mwingine wa kisheria kwakuwa sheria ya kuanzisha mchakato wa katiba inataka rasimu ikitoka Bungeni ipelekwe kwa wananchi ndani ya miezi sita.

Jumamosi, 4 Oktoba 2014

Hii ni kuhusu Wanajeshi kupigana na Polisi Tarime juzi, wangapi wameumia? kisa?

mhabari forum blog spot.comHii ni taarifa kutoka Tarime mkoani Mara ambako watu 12 wamejeruhiwa wakati wa mashambulizi ya kurushiana risasi kati ya askari wa JWTZ kituo cha Nyandoto na polisi wa kituo cha stendi.
Kwa mujibu wa magazeti ya Nipashe na Mwanachi leo, hii ishu ilitokea wakati Wanajeshi hao walipokua wakijaribu kumchukua Mwanajeshi mwenzao aliyekamwatwa na polisi hao kwa kosa la kuendesha pikipiki bila kuvaa kofia (Helmet).
Mashambuliazi hayo ya kurushiana risasi na kupigana ngumi na mateke yalitokea juzi jioni katika kituo hicho cha stendi ambapo Mganga Mfawidhi Hospitali ya Tarime alithibitisha kupokea majeruhi 12 na kati yao wawili ni askari wa JWTZ, Polisi saba na raia watatu.
Kamanda wa Polisi Tarime alisema Mwanajeshi huyo licha ya kukiuka taratibu za barabarani aliwatolea lugha za matusi polisi hao jambo lililowalazimu kumkamata kwa nguvu na wanajeshi wenzake kuingilia kati na kusababisha vurugu.
Alisema Wanajeshi watatu ambao hawakutajwa majina wameshikiliwa na polisi kwa kuvunja utaratibu wa usalama huku Mkuu wa Wilaya hiyo John Henjewele akilaani kitendo hicho cha kurushiana risasi za moto hewani na kusema ni cha utovu wa nidhamu na kilikwamisha shughuli za watu kwa muda sababu ya kuhofia usalama wao.