Mpasuko wa ndoa ya wasanii wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha
na mkewe Florah umewagawa wachungaji wa makanisa mbalimbali
nchini baada ya kibao kumgeukia Flora kwamba ndiye anadaiwa
kusuka mpango wa kumwangamiza mumewe ili afungwe kwa kosa la
ubakaji…..
Wakizungumza na wanahabari wetu kwa nyakati tofauti, wachungaji
hao walisema endapo itabainika ni kweli Flora ameshiriki
kumsaliti mumewe kwa kutembea na mmoja wa wachungaji maarufu
nchini hapatakuwa na haja ya kumwalika kwenye huduma zao kwani
hawawezi kuhudumiwa na mwimbaji mzinzi.
Mchungaji Ambonile Mwakipesye na Amani Joseph wa makanisa ya
Tanzania Assemblies of God ( TAG) walisema kuwa kama kulikuwa
na matatizo kwenye ndoa yao walipaswa kuwaona watumishi wa
Mungu na kusuluhisha badala ya kutengenezeana mitego na
kuingizana majaribuni kama inavyodaiwa kutokea kwa Mbasha….
Wakati wachungaji hao wakisema hivyo, mchungaji Thomas Methew
yeye alisema kuwa ukweli wa jambo hilo wanaujua wanandoa
wenyewe kwani mpaka sasa hakuna anayelijua tatizo kubwa mpaka
wakafikia hatua ya kutengana
0 maoni:
Chapisha Maoni