Stori: Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
IMEBAINIKA kuwa miongoni mwa wale wanawake 20 waliodai kufanyishwa ngono
na waganga wa kienyeji ‘sangoma’ ili kupata ujauzito baada ya kukaa
muda mrefu bila watoto, wamo wake wa vigogo Bongo, Uwazi limechimba.
Uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu kwa baadhi ya wanawake hao
umebaini kuwa, waume wao wanafanya kazi katika nyadhifa za juu
serikalini, wengine ni wastaafu na kwamba waume hao hawajui
kinachoendelea.
Kwa mujibu wa mwanamke mmoja (jina lipo), katika sakata hilo kuna wake
wa maprofesa, kanali mstaafu wa JWTZ na mmoja ambaye mume wake aliwahi
kuwa kamanda wa polisi wa mkoa (RPC) ambaye kwa sasa naye ni mstaafu.
Mwanamke huyo alizidi kudai kuwa, ndoa moja katika hizo ilivunjika baada
ya mume kubaini kuwa, mkewe alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmoja
wa sangoma hao.
‘KUFULI’ ZILISHATUMIKA
Uchuguzi zaidi ulibaini kuwa zaidi ya nguo za ndani ‘kufuli’ za
wanawake zaidi ya 20 zilizokutwa na polisi kwa sangoma hao maeneo ya
Tandika jijini Dar es Salaam zilikuwa zimeshavaliwa hivyo hakukuwa na
mpya jambo lilionesha kuwa, zilivuliwa wakati wa tukio linalodaiwa
lilikuwa na kutengezea dawa.
KWA NINI WALITOA TAARIFA POLISI?
“Sisi tuliamua kutoa taarifa polisi kwa sababu tumekuwa tukifanya ngono
na wale waganga kwa muda mrefu bila kupata ujauzito na mbaya zaidi
tulishatumia mamilioni ya pesa baada ya kuuza mali zetu, zikiwemo
nyumba,” alisema mwanamke huyo nje ya kituo cha polisi.
Wanawake hao ambao hawakupenda majina yao yatajwe kwa kuhofia waume zao
kujua, walisema ni kweli baadhi yao wamekaa katika ndoa kati ya miaka
nane hadi 10 bila kupata watoto wala mimba zilizoharibika.
Hata hivyo, baadhi yao walirudishiwa fedha zao baada ya Kamanda Kiondo kuwabana waganga hao.
KAULI YA RPC
Wiki iliyopita Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke chini ya Kamanda, SACP
Englibert Kiondo liliwatia nguvuni sangoma wawili wakiwa na matunguli na
zana nyingine za kuagulia binadamu.
Vitu hivyo viliteketezwa moto kwenye Kituo cha Polisi Temeke mbele ya waandishi wa habari.
“Ninaamini kuwa kwa vitendo hivyo vya kujamiiana ni hatari na huu ni
ubakaji, kwani kuna uwezekano wa kuambukizana maradhi mbalimbali
ikiwemo Ukimwi, kwa hiyo hizi zana nazichoma moto,” alisema Kamanda
Kiondo.
Waliokamatwa katika zoezi hilo ni Juma Mohamed (32) na Abdallah Musa (25) ambao wote kwa pamoja wanashikiliwa na jeshi hilo.
GPL
0 maoni:
Chapisha Maoni