18 Juni, 2014 - Saa 11:23 GMT
Shirikisho la soka nchini Ghana,
limekanusha ripoti za kituo kimoja cha redio nchini humo kwamba timu ya
taifa ambayo inashiriki michuano ya kombe la dunia imekumbwa na
mgawanyiko hasa baada ya kushindwa na Marekani mabao mawili kwa moja
Jumatatu.
Kulingana na kituo hicho cha Joy FM, huenda
wachezaji wamegawanyika na kumkataa kocha mkuu, hali ambayo ililazimisha
maafisa wa timu hiyo kufutilia mbali mkutano waliokuwa wameandaa na
waandishi wa habari Jumanne."hakuna mchezaji hata mmoja ametofautiana na kocha Kwesi Appiah."
Taarifa hiyo iliongeza kusema, "hakuna mchezaji au wachezaji wamehusika na njama ya kukataa kucheza pamoja na kumpinga kocha mkuu. ''
"mkutano ambao tulikuwa tumeandaa na wandishi wa habari ambao ulipangwa kufanyika saa tano saa za Brazil, ulikuwa wa wasimamizi wa timu wala sio wachezaji. Ulibadilishiwa muda na kupangwa kufanyika saa kumi na nusu jioni kwa sababu kikosi kilikuwa kimeswali kuchelewa.''
Wachezaji wote 23 wa timu ya taifa ya Black Stars, walikuwepo tayari kwa mkutano kwa mwongozo wa Appiah.
Tunataka kuwahakikishia wananchi wa Ghana kuwa kocha Kwesi Appiah na wachezaji wake, wanaangazia zaidi mechi yao dhidi ya Ujerumani wiki ijayo, na wako makini kushinda mechi hiyo.
Baada ya mechi ya Ujerumani, mechi ya mwisho ya Ghana itakuwa dhidi ya Portugal Alhamisi wiki ijayo.
0 maoni:
Chapisha Maoni