Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
MAHAKAMA kuu kanda ya Moshi imetoa adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa washtakiwa wawili raia wa Kenya katika kesi ya mauaji ya askari Polisi, Pc Michael Milanzi, wakati wa tukio la uporaji wa fedha katika benki ya NMB tawi la Mwanga mkoani Kilimanjaro. Mbali na hukumu hiyo iliyosomwa na Jaji mfawidhi wa Mahakama kuu, Kakusulo Sambo kwa zaidi ya saa, nne ,Mshatakiwa wa tatu katika kesi hiyo ,Karisti Kanje(Mtanzania) yeye amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitano(5) jela kwa kosa la kuhifadhi na kutorosha watuhumiwa wa mauaji ya askari polisi.
Vichwa vya Habari Zaidi
6 days ago
Mwananchi 12 JunWizi NMB Mwanga: Wakenya wawili wahukumiwa kifo
Raia wawili wa Kenya, Samweli Saitoti (Saimoo) na Michael
Kimani (Mike), wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na
hatia ya kumuua polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), PC Michael
Milanzi mwaka 2007.
6 days ago
Tanzania Daima 12 JunWezi NMB kunyongwa
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Moshi, imetoa adhabu ya kunyongwa
hadi kufa kwa washitakiwa wawili raia wa Kenya, waliokuwa wakikabiliwa
na kesi ya mauaji ya askari polisi PC Michael Milanzi. Washitakiwa...
6 days ago
Uhuru Newspaper 12 JunWaliopora NMB wahukumiwa kifo
NA WILLIUM PAUL, MOSHI
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Moshi, imewahukumu raia wawili wa Kenya, kunyongwa hadi kufa baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kumuua kwa kukusudia askari Polisi, wakati wa tukio la uporaji la Benki ya NMB, Mwanga.
Wakati Wakenya hao Samwel Saitoti na Michael Kimani, wakipewa adhabu hiyo, Mtanzania Calist Kanje alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kuwa mshiriki mkuu.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kakusulo Sambo, alisema baada ya kusikiliza na kutafakari ushahidi uliowasilishwa na mashahidi 18 wa upande wa Jamhuri, mahakama imeridhika kuwa upande wa Jamhuri umethibitisha mashitaka dhidi yao pasi kuacha shaka yoyote.
“Kutokana na ushahidi wa mashahidi wa kwanza, watatu na wa 11, mahakama imeridhika kuwa Saitoti na Kimani ambao ni raia wa Kenya, walimuua kwa makusudi Konstebo wa Polisi, Michael Milanzi kwa kumpiga risasi, hivyo inawaoa adhabu ya kunyongwa hadi kufa,” alisema.
Jaji huyo, alisema washitakiwa hao kwa pamoja wakiwa na lengo la kutekeleza ujambazi katika benki hiyo, waliamua Michael kitendo ambacho kisheria adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa.
Pia, alisema baada ya kutafakari kwa kina maelezo ya Jamhuri pamoja na ya mashahidi wa 8, 16 na 17, mahakama imeridhishwa kuwa mshitakiwa huyo, raia wa Tanzania, alikuwa ni mshirika mkuu wa washtakiwa hao.
Alisema kutokana na ushiriki wake huo, mahakama hiyo inamhukumu mshitakiwa huyo kifungo cha miaka mitano kwa kosa la kuhifadhi na kutorosha watuhumiwa wa mauaji ya askari Polisi huku akifahamu kuwa ni kosa kisheria.
Aidha, mahakama iliamuru fedha ambazo walikutwa nazo washitakiwa hao ambao ni Dola za Marekani 8145 na fedha za Tanzania sh. milioni 1.7 zikabidhiwe kwa benki ya NMB, Mwanga.
Wasitakiwa hao wote walikuwa wanakabiliwa na shitaka la mauaji ya kukusudia ya polisi huyo, ambapo ilidaiwa wakiwa na wenzao wengine 9, walishiriki katika tukio la uporaji na mauaji yaliyotokea Julai 11, mwaka 2007 katika Benki ya NMB tawi la Mwanga, wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro.
Raia hao wa Kenya, tayari wanatumikia kifungo kingine cha miaka 67 jela baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kuwatia hatiani kwa kosa la kula njama na kupora sh.million 239 katika tukio la wizi kwenye benki hiyo.
Saitoti na Kimani walitiwa hatiani kwa kosa hilo na kufungwa kwenda jela miaka 30 kila mmoja huku Mtanzania mwingine Elizabeth Msanze au “Bella”, akihukumiwa kifungo cha miaka saba jela.
2 months ago
GPLWALE WALE REMIX - KALA JEREMIAH FT JUMA NATURE, YOUNG KILLER & NAY LEE
WALE WALE REMIX - KALA JEREMIAH FT JUMA NATURE, YOUNG KILLER &
NAY LEE
DIRECTED BY: PABLO D360 VIDEOS
PRODUCED BY: ZEST & PADY MAN, PLEXITY…
DIRECTED BY: PABLO D360 VIDEOS
PRODUCED BY: ZEST & PADY MAN, PLEXITY…
4 months ago
Tanzania Daima 28 FebNMB yafungua tawi Tabata
BENKI ya NMB imefungua tawi jipya maeneo ya Tabata,
Barabara ya Mandela, Dar es Salaam. Ufunguzi wa tawi hilo la 20 jijini
hapa umekuja ili kuongeza wigo wa matawi ya...
0 maoni:
Chapisha Maoni