More Giniazy track

[soundcloud url="https://api.soundcloud.com/tracks/167825674" params="auto_play=true&color=ff5500" width="100%" height="166" iframe="true" /]

Alhamisi, 19 Juni 2014

SOMA HABARI NYEPESINYEPESI NA ZA KUSISIMUA DUNANI KOTE HAPAA

 Mwanamke mmoja wa Ufaransa KLOR BOR amepata ujanja wa kuwapa mwamko wanachi wa mji mkuu wa nchi hiyo Paris dhidi uharibifu wa vipande vya sigara vilivyomalizika kuvutwa ambavyo vinatupwa tupwa ovyo njiani hasa ktk mitaa iliyokaribu na maeneo ya treni ya chini ya ardhi yaani Metro. Mwanadada huyo ametengeza vazi la sketi alilolitengeneza mwenyewe kwa maelfu ya vipande vya sigara.                                        
 ***kionjo*** Umuhimu mkubwa wa afya nchini Italia sio kwa binaadam peke yake, bali mpaka miti imepewa kipaumbe ktk kuwa na afya nzuri. Nchini humo miti midogo2 imezungushiwa kipande cha kitambaa chepesi kwa ajili ya kuihifadhi miti hiyo isipigwe na baridi ya hali ya hewa, ili iweze kukua vizuri ktk mazingira yake ya kiasili. Lakini cha ajabu zaidi ni kuwa vitambaa vilivyozongewa miti hiyo vina rangi ya kijani ili miti hiyo isitOfautiane na mengine.                                                                                                                                                                                                                                                                                 Aina ya ajabu ya mazoea mabaya yaliyomkumba Mmarekani aitwae PITAMIST HANDERSON ambayo yanamsababishia kula sabuni na shampoo za kukogea tokea alipokuwa mtoto mdogo. Hapo mwanzo alikuwa anapenda harufu na hatimaye mapenzi yameongezeka zaidi na akaamua aonje ladha ya sabuni hizo. Baada ya kuonja ikampendezesha ladha na akaendelea kula sabuni hizo mpaka akawa na mazoea nazo hadi leo hii. Na anakula vipande vitano vya sabuni kwa wiki. Na baada ya kupita miezi kadhaa ya mazoea haya ameamua kuomba msaada wa madaktari ili aondokane na mazoea haya.                                                                                                                                                                                                                              Na ktk habari za kusisimua kabisa ….. ni kuwa kitabu kimoja chenye jina la “MAMBO YANAYOWASHUGHULISHA MNO WANAUME” kilichotungwa na profesa SHARIDAN SAIMON kimetawala mitaani. Cha kushangaza ni kuwa … kurasa za kitabu hichi ni tupu yaani hazijaandikwa hata neno moja wala picha wala alama yoyote ile. Lakn kwa namna ya ulivyo muundo wake wa kuvutia kati ya anuani na vilivyomo ni muundo haujawahi kukuwepo hapo kabla. Kitabu hichi kimepanda chati na kuwa miongoni mwa vitabu vilivyouzwa sana na kimekuwa juu hata kuvishinda baadhi ya vitabu mashuhuri duniani. Na hatimae nchini Marekani wakati mkimbiaji MERY mwenye umri wa miaka 72 ameshinda vita vilivyokuwa vikali kati yake na mamba, akipigania kumuoko mbwa wake kutoka ktk kinywa cha mamba. Kwani alimuona mbwa wake aitwae JERY mwenye miaka 11 yupo kinywani mwa mamba. Akaamua kumrukia mamba huyo mgongoni na kuanza kumpiga kichwani mpaka akamuacha mbwa wake. Na akafanya haraka kumkimbiza hospitali ambapo alipatiwa matibabu. Na Mery amesema yeye sio shujaa, bali jambo kubwa alilolitaka ni kumuokoa mbwa wake.

0 maoni:

Chapisha Maoni