More Giniazy track

[soundcloud url="https://api.soundcloud.com/tracks/167825674" params="auto_play=true&color=ff5500" width="100%" height="166" iframe="true" /]

Jumapili, 22 Juni 2014

Matusi Ya Instagram Yamliza Wema Sepetu Kwa Kumtaja Mama Yake


Wema Abraham Sepetu ameeleza jinsi alivyoumizwa na matusi makali yaliyoporomoshwa na mashabiki wa team pinzani (team za Instagram) dhidi yake, matusi ambayo yamemtaja mama yake mzazi.
Wema na mama yakeMuigizaji huyo ameeleza hisia zake kama mtoto anaemjali na kumpenda mama yake mzazi, anaeumizwa pale mama yake anapoingizwa kwenye ugomvi wake usiomhusu na kuvunjiwa heshima kwa matusi.
Wema ameandika kwenye Instagram:
Dah…! Sijui hata niseme nini…! Ila si mlitaka kuniumiza… leo mmefanikiwa… nawapeni hongera…. Tena mmetisha haswa… Kila sjku huwa hata siumizwi na matusi yenu cuz naonaga kama ni mnajisumbua tu… Hakuna siku nimelia kwa uchungu kama leo… I min mnitukane mimi mpaka mchoke but leave my mum out of it… Kawakosea nini nyinyi mama angu mpaka mfanye hivyo… Mzazi nwenyewe ndo nimebakia nae mmoja tu… mnataka afe na yeye nibaki yatima sio… dah… leo mmeniweza… saana jamani… Basi naomba isifike huko… nina uchungu sana na mama angu … nampenda sana mama angu ila naona mnataka kuniulia mama angu… Picha halisi ndo hio hapo juu kweli mtu uende ukamfanyie hivyo mama wa mwenzako… una mama wewe.. au uliokotwa na hujui uchungu wa mama… dah… nime surrender leo…. hongera zenu narudia tena… mmeniweza leo…. dah… Mungu nipe nguvu ktk hili jamani… Kwani nilichokikosea haswa ni kitu gani mpaka iwe hivi . Nimekosa nini mimi yarabi toba…. Eeeh mungu… Dah… Ila nashkuru….

0 maoni:

Chapisha Maoni