Idadi ya watu waliuliwa katika shambulio la kigaidi kwenye jengo
la maduka la Westgate mjini Nairobi, Kenya imefikia 68. Shirika la
Msalaba Mwekundu nchini humo limetangaza kuwa, idadi hiyo imeongezeka
baada ya kupatikana miili ya watu wengine tisa na hivyo kuifanya idadi
hiyo kufikia 68. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari zaidi ya watu 200
wanaripotiwa kujeruhiwa katika tukio hilo. Hadi jana serikali ya Kenya
ilikuwa imetangaza kuwa kwa akali watu wenye silaha wapatao 10 hadi 15
walikuwa bado wamo katika jengo hilo la biashara huku wakiendelea
kuwashikilia watu wapatao 36. Jeshi la Kenya kwa kushirikiana na askari
kutoka nje ya nchi hiyo, limetangaza kuwa, linafanya juhudi ya
kuhakikisha linawatia mbaroni watu hao wenye silaha na kuwaokoa mateka
wengine wanaoendelea kushikiliwa. Hii ni katika hali ambayo Waziri wa
Mambo ya Ndani wa Kenya ametangaza kuwa watu wasiopungua elfu moja
tayari wameokolewa hadi sasa. Wakati huo huo msemaji wa kundi la kigaidi
la ash-Shabab ametoa taarifa na kukiri kuhusika kundi hilo na
shambulizi hilo la Westgate huko Nairobi.
Jumanne, 17 Juni 2014
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 maoni:
Chapisha Maoni